Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”.
Ni agizo la Mungu kwam

Unaona hapo? Biblia inasema pia ukiweza kuuzuia ulimi wako hata SIKU YAKO ITAKUWA NJEMA…na ndivyo utakavyopata amani..Yakobo 3:5 “Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.
6 Nao ULIMI NI MOTO; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum”
Hivyo mara zote tukijifunza kukaa kimya na kuwa wapole na wenye busara…basi ni lazima tu tutakuwa na amani na watu wote….Sisemi kwamba hautakuwa na watu wanaokuchukia kabisa,…hapana watu wanaokuchukia watakuwepo tu! lakini hawatakuwa na la kufanya kwako kwasababu muda wote watakuona ni mtu wa amani. Watatafuta maneno kwako lakini hawatayapata…hivyo mwisho wa siku wataachana na wewe, na kuendelea kufikiri mambo yao mengine.1Petro 3:10 “Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila.
11 Na aache mabaya, atende mema; ATAFUTE AMANI, aifuate sana”
Lakini ukiwa ni mtu wa kujibiza, kamwe vita kwako havitaisha..na hakuna siku utapata amani…kama mtu akikuudhi wewe nawe unajibu mashambulizi kwa kumrudishia maneno…nataka nikuambia hakuna siku utakuwa na amani, utakuwa ni mtu wa kugombana tu kila siku, na wa kukosa raha, na muda mwingine kuweka vinyongo tu…na pasipo kujua kuwa tatizo kubwa lipo upande wako.
Kila mahali jaribu kuwa mpole…hiyo ndiyo njia ya kupata Amani na watu wote…Na kuwa mpole sio “udhaifu”….Bwana wetu Yesu alikuwa ni mpole(Mathayo 11:28) na mtu mpole mara nyingi sio mtu wa kuzungumza sana, na sio mtu wa kuzungumza mambo ya wengine (msengenyaji).Mithali 15:1 “Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu”.
Sisi kama wakristo tukiudhiwa kwa maneno sio lazima tujibu neno,.. ukiumizwa hupaswi na wewe kumuumiza..kila wakati tafuta namna ya kulitatua tatizo badala ya kulichochea…na kwa jinsi utakavyoonesha bidii ndivyo Mungu atakavyozidi kukupatanisha na wale ambao wanaonekana ni maadui zako wa kudumu..Na hivyo utazidi kuwa na amani.Wafilipi 4:5 “Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu”.
Hivyo Bwana anavyotuambia tutafute kwa bidii (maana yake tufanye kila tuwezalo) tuwe na amani na kila mtu, kama vile tunavyofanya bidii kuutafuta utakatifu ambao hakuna atakayemwona Mungu asipokuwa nao.Mithali 16:7 “Njia za mtu zikimpendeza Bwana, Hata adui zake huwapatanisha naye”.
Shalom.
https://wingulamashahidi.org/