Rupia aubuka mchezaji bora ligi kuu FKF Disemba

Mshambulizi wa AFC Leopards Elvis Rupia ametawazwa mwanasoka bora kwenye ligi kuu ya FKF Kenya mwezi Disemba mwaka jana .


Rupia aliwapiku kipa wa KCB Joseph Okoth na mshambulizi wa Kariobangi Sharks Eric Kapaito na kuwa mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo inayoandamana na shilingi 50,000.


Mshambulizi huyo alikuwa na msimu bomba akipachika wavuni maboa 6 katika mechi 4 za ufunguzi kufikia Disemba akifunga bao moja katika ushindi wa Leopards wa mabao 2-1 dhidi ya Tusker FC,na kufunga mengine mawili dhidi ya Bidco United kabla ya kufunga magoli 3 dhidi ya Sofapaka .


Tuzo hiyo itakuwa ikitolewa kila mwezi ikiwashirikisha kocha na mchezaji bora.

20210212-35991.jpeg
 

Mishale

Elder Lister
wacha tuombe hakutakua na kesi za wanao chagua mshindi kutaka hongo/rushwa kutoka kwa wanao wania tuzo hilo ili washinde.
 
Top