Atilax paludinosus

Meria

Elder Lister
Staff member
312169343_1499098953837516_1797531851356233031_n.jpg
312126715_1499098877170857_4228772563400976702_n.jpg

Huyu ni Nguchiro,kwa jina lingine anaitwa Kicheche, kwa kiingereza anaitwa Mongoose ,japo ni wanyama wastani kwa kimo ni weledi kwa kuwinda na kuua nyoka , ,nyoka na Ndege ndio baadhi ya vyakula bora kwao, ,wanao uwezo wa kuua nyoka wa aina yote, kama vile Bafe na Swila, ni Anakonda na Chatu pekee, ndio mababe kwake
Sasa kuna spishi nyingine ya Nguchiro waitwao Vansire au pia Nguchiro wa maji, Yaani Water Mongoose, jina lao la kisayansi ni Atilax paludinosus, wao wana njia yao mahsusi ya kuwanasa kuku au ndege yeyote mwenye tamaa ya nyama,
Kwanza kabisa wao kujibanza Mahali kichakani kisha kulala chali kama walalavyo watalii ufukweni Mwa bahari Hindi kule pwani, huku akiwa ameifungua wazi 'ufunguo wa tumbo' wenye rangi ya waridi (pink) atajifanya ameikata roho huku akisubiri ndege au kuku mwenye tamaa ya kuionja mnofu ajilete na tamaa zake, asijue ni Mtego na kwamba kiama chake kipo njiani, sasa Mara tu atakapojaribu kuidona, kuta za Babeli zinafungwa, inabakia kubwebwa,, hakuna, kupiga kamsa, hakuna kupumua nk
cc @bigDog - kwa gikuyu tunamuita aje? 50mrks.
 
Top