ANAOMBA USHAURI

kitela5

New Lister
ANAOMBA USHAURI.
Mimi naitwa Debora, nina miaka kumi na sita lakini
shida nazokutana nazo Mungu ndiye anajua,, kwanza
kabisa nasoma kidato cha pili na nina na
mwanaume wangu ninampenda sana yeye ana
miaka 25, hasomi wala hana shughuli yoyote,
kinachonifanya nimpende huyu kaka ni kwamba
anajua sana mapenzi yaani yupo romantic balaa pia
ndiye aliniiingiza katika ulimwengu wa mapenzi kwa
ufupi siwezi kumuacha.. Tatizo lake sasa kila kitu
ananitegemea mimi kwa sababu natoka familia
yenye uwezo kidogo, kila kitu ni mimi namnunulia
kuanzai nguo za ndani haki kula kila siku, mimi
nadanganya kuchukua hela za uongo nyumbani
kumbe napeleka kwa mwanaume jamani, sasa
mzigo umenizidi kwa sababu juzi juzi kaniomba
hela apange chumba nikajitahid kumdanganya baba
akanipa laki tatu nikampa amepanga chumba
nimefanya kazi ya kununua godorolakini juzi juiz
nimepata fununu kuwa kuna mwanamke Fulani
anaingia anye pale chumbani, jamani sijui nifanyeje
kuna rafiki yangu ananishauri nikamshaki polisi
lakini mimi nampenda sitaki kumpoteza kwani
tumepanga mengi sana katika maisha yetu, nilitaka
tu nikimaliza kidato che nne tuoane. Je mnanishauri
vipi ndugu zangu ??
 
Top