Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia

john7

Lister
download-7.jpg


SWALI: Nini maana ya huu mstari? Mithali 11: 15 “Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia; Achukiaye mambo ya dhamana yu salama”.


*JIBU* : Biblia ni kitabu pekee ambacho kinamfundisha mtu kutembea katika kanuni zote (yaani za mwilini na rohoni), jinsi ya kuishi katika roho, vilevile na jinsi ya kuishi katika mwili, Na moja ya kitabu ambacho kinatufundisha kanuni za kutembea katika mwili na kufanikiwa ni hichi kitabu cha Mithali,

Ni kitabu ambacho kina mahusia kwa makundi yote ya watu kuanzia wanandoa, vijana, watoto, maskini, matajiri, vilevile kina maonyo kwa viongozi, hadi kwa watumwa, Hivyo, tukirudi katika swali, kwanini Sulemani kwa hekima ya Roho alisema.. “Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia; Achukiaye mambo ya dhamana yu salama”.

Hapo Hakumaanisha kuwa, kumdhamini mtu yeyote, ni kosa, hapana, bali anatoa angalizo katika kutoa dhamana kwa mtu mgeni (usiyemfahamu), kunaweza kukuweka katika hatari kubwa sana ya kukumbana na shida. Kumchukulia mtu mkopo bank halafu, unaweka nyumba yako rehani, mtu ambaye umekutana naye kwa kipindi kifupi tu, bado hujui vizuri mwelekeo wake upoje, halafu unaweka mpaka na mali zako rehani, hapo ni rahisi sana kuishia pabaya,

Hatupaswi kukurupuka kumdhamini mtu, ili mradi tu mtu kisa tunafanya tendo jema. Hapana kinyume chake biblia inaturuhusu tuchukue muda wa kumtambua, kumfahamu, kumwelewa, ndipo tumdhamini kama kuna umuhimu wa kufanya hivyo, Lakini Zaidi sana tukibaki kama tulivyo, tukamwachia Mungu asimamie mambo hayo ya kudhamini, tutakuwa katika upande ulio salama Zaidi. Kwasababu bado wakati mwingine mtu anaweza akawa ni mwema kweli, au akawa na mwelekeo mzuri lakini kwa bahati mbaya mambo yakabadilikia ghafla njiani, labda kapata hasara, hapo atakayeumia ni wewe uliyemdhamini.

Na ndio maana bado Biblia bado inasisitiza suala hilo hilo katika vifungu vingine mbeleni kidogo inasema..

Mithali 22:26 “Usiwe mmoja wao wawekao rehani; Au walio wadhamini kwa deni za watu; 27 Kama huna kitu cha kulipa; Kwani ukaondolee kitanda chako chini yako?”

Lakini maneno haya yanatufundisha nini rohoni?

Yupo ambaye hakuogopa jambo hilo, aliingia katika hii hatari ya kutudhamini, huku akijua kabisa, anaowadhamini hawawezi kulipa madeni yao hata kidogo, lakini alijiingiza katika shida zao, na kwa nguvu zake, akafanikiwa kulipa makosa yetu yote.

Angeweza kuacha asitudhamini, kwasababu maandiko yametoa ruhusa hiyo kama tulivyosoma.. Lakini kwa upendo wake, usiopimika, alikubali kulipa madeni yetu yote. Na huyo si mwingine Zaidi ya Bwana wetu YESU KRISTO.

Hakika sifa heshima na utukufu vina yeye, milele na milele. Amina.

Ni kitendo cha kushangaza sana na cha aibu, kuona mpaka sasa kuna baadhi ya watu wapo nje ya neema yake.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

+255693036618
 
Top