Huku DRC

Meria

Elder Lister
Hiyo ilitokea juzi tarehe 22 Jan 23 katika eneo la Salamabila lililoko Jimbo la Maniema nchini Kongo. Hao wenye bunduki ni wanamgambo wa kundi la Mai Mai Malaika. Wameamriwa na kiongozi wao Sheikh Kabala Selemani kuwachapa viboko wanawake na wasichana wote wanaovaa suruali na nguo fupi zikiwemo zinazoonyesha maumbile yao, na ukiwa mchafu. Vijana wachafu na wanaovaa mlegezo nao ni fimbo. Wanafunzi wakikutwa nje wakati wa masomo ni fimbo, Mwalimu mkuu akiwaambia wanafunzi waende na viti shuleni ni fimbo. Wanawake walioolewa wakibainika kufanya uzinzi ni fimbo kali, hii ni pamoja na machangudoa.
 
Back
Top