Nani alitumia hii

MbitikaZetu

Elder Lister
Yetu ilikuwa ya mbao. Ilikuwa na miguu kama stool. Heheheee... Ilikuwa imeandikwa national. Ilikuwa inafunikwa kitambaa... Kuna button ilikuwa inazungushwa from 1 to 10 ati kuchange channel. 1 ilikuwa inashika VOK, na 7 ilikuwa inashika tu hiyo hiyo VOK.. Zile zingime zilikuwa za mchele. Ukiwasha ulikuwa unategea kwanza, ama unaenda kupika chai ama unakula njaro tu huko nje ukirudi ndio utapata picha imeiva, otherwise sauti ilikuwa inaanza tu immediately unaskiza kama redio. Saa zingine Jacob William Maunda akisoma news alikuwa anapanda pole pole kwa screen hadi huko juu, huku Maunda mwengine akimfuata kutoka chini polepole mpaka huyo wa kwanza anapotea, huyo wa pili anaruka ghafla na kutulia kwa screen. Saa zingine hatulii wanatokea wengi wanaaanza kufukuza kwa tv kutoka chini juu. Haraka haraka. Polepole. Halafu mmoja anatulia. Ukizima ilikuwa inatoa kiflash kama lightning halafu inaacha kabright spot hapo katikati. Ilipelekwa kwa fundi na haikuwahi rudi. I miss that thing.

Favourite ilikuwa urtna (music), big daddy (wrestling) na sesame street. Vitimbi ilikuwa inaniboo mbaya
That was in the 80s and early nineties. I recall with nostalgia those times.
 
Top