NA YEYE ALIYEKETI JUU YA WINGU AKAUTUPA MUNDU WAKE JUU YA NCHI, NCHI IKAVUNWA.

john7

Lister
Jina la Bwana Yesu libarikiwe. Karibu tujifunze maneno ya uzima.


Biblia inasema..



Ufunuo 14:14 “Kisha nikaona, na tazama, wingu jeupe, na juu ya wingu hilo ameketi mmoja, mfano wa Mwanadamu, mwenye taji ya dhahabu juu ya kichwa chake, na katika mkono wake mundu mkali.
15 Na malaika mwingine akatoka katika hekalu, akimlilia kwa sauti kuu yeye aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu, Tia mundu wako, ukavune; kwa kuwa saa ya kuvuna imekuja; kwa kuwa mavuno ya nchi yamekomaa.
16 Na yeye aliyeketi juu ya wingu akautupa mundu wake juu ya nchi, nchi ikavunwa”.
Ndugu saa ya mavuno, ipo karibu sana..tena Sanaa.. Utauliza tunajuaje kuwa ipo karibu? Tunajua kutokana na jinsi tunavyoona magugu na ngano yanavyojitenga kwa kasi katika kanisa la Mungu, na katika dunia kwa ujumla. Baadhi ambao walikuwa wanasema huyo Yesu mbona hahukumu dunia, nataka niwaambie wapo kwenye uwezekano mkubwa sana wa kukumbana na hukumu hiyo wakiwa bado hai, kama hawatageuka..


Hawajui kuwa Siri ya Mungu ya kutowahukumu waovu tangu zamani, imejificha ndani ya ule mfano wa magugu na ngano ambao Bwana Yesu aliutoa kwa makutano, embu tusome kidogo..



Mathayo 13:24 “Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake;
25 lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.
26 Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu.
27 Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu?
28 Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye?
29 Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing’oa ngano pamoja nayo.
30 Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.
Click to expand...
saa ya mavunosaa ya mavuno

Na tafsiri yake ilikuwa ni hii..



37 Akajibu, akasema, Azipandaye zile mbegu njema ni Mwana wa Adamu;
38 lile konde ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu;
39 yule adui aliyeyapanda ni Ibilisi; mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika.
40 Basi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia.
41 Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi,
42 na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Hakuyang’oa magugu, kwasababu magugu yakiwa machanga ni ngumu kuyatambua, yanafanana sana na ngano.


Vivyo hivyo Zamani ilikuwa ni ngumu sana kuwatambua watu ambao ni mashoga katika kanisa la Kristo, Lakini leo hii tunawaona tena wana vyama vyao na viongozi wao katika hayo wanayoyaita makanisa yao. Zamani, ilikuwa ngumu kuona mtu anayejiita mkristo halafu ni mzinzi, lakini leo hii utawaona tena kwa mavazi yao ya kikahaba , utaona waasherati wazi wazi katika nyumba ya Mungu, na wengine wanajiita wachungaji na manabii…Wahuni ilikuwa ni ngumu kuwajua ndani ya kanisa, lakini leo utawaona wazi wazi..n.k


Mambo hayo kama ukifuatilia historia utaona Kuanzia karne ya 19 kushuka chini, hayakuwepo kabisa,..Vilevile dunia nzima ilikuwa inaamini walau kuna kitu kinachoitwa Mungu..Lakini leo hii, utaona wimbi kubwa la watu ulimwenguni lisiloamini Mungu kabisa..Hiyo ni ishara kuwa ngano na magugu tayari yameshajitenga, na kukomaa..Ulikuwa huwezi kuona mkristo anajihusisha na miziki ya kidunia, lakini leo hii utawaona kwa staili za uimbaji wao..


Utajiuliza ujasiri wote huo wameutolea wapi?.. Sio ujasiri, bali ni magugu yamekomaa sasa, yanajitofautisha na ngano halisi za Mungu. Haziwezi kuishi Maisha matakatifu kwasababu zenyewe hazikuwa ngano tangu awali, mwanzoni zilijifanya tu kama wakristo ili zipate hifadhi ya mvua ya neema, lakini sasa zimeshakua hazihitaji tena kujificha..


Na hiyo ndio inayokwenda kupelekea wavunaji (malaika) wa Bwana, waje kuuvuna ulimwengu huu wakati sio mwingi.


Wawafunge matita matita, kabla ya kwenda kuwateketeza kwenye lile ziwa la moto. Na hiyo inakuja pale mtu anapohubiriwa njia ya kweli lakini anashupaza shingo yake, wale malaika wanachofanya ni kumtia muhuri, ambayo ndio Kamba yenyewe. Sasa Hilo likishakutokea basi mtu huyo ni ngumu kumgeukia Mungu, ataendelea kuwa hivyo hivyo mkaidi, mpaka mwisho…


anachosubiria ni hukumu tu ya mwisho. (Na hiyo ni kulingana na maandiko na sio kumhukumu Mtu). Wokovu hauna uvuguvugu..


Hichi si kipindi tena cha kuishi Maisha ya kutokujali, si wakati wa kufurahia maovu kanisani, si wakati wa kuiga kila staili ya Maisha inayozuka ulimwenguni, si wakati wa kupokea kila aina ya elimu za uongo zinazohubiriwa na manabii wa uongo, Huu si wakati wa kushikilia dini, Bali Ni wakati wa kuujenga uhusiano wako wewe na Mungu. Kabla ya nyakati za hatari hazijafika..


Kumbuka..Yule malaika alimbiwa..


Tia mundu wako, ukavune; kwa kuwa saa ya kuvuna imekuja; kwa kuwa mavuno ya nchi yamekomaa.


Kipindi chenyewe ndio hichi.. Je! Unasubiria uwekwe kwenye kundi la magugu? Kama sivyo basi yasalimishe Maisha yako kwa Kristo na yeye atakuponya. Kimbilia msalabani upate wokovu wa kweli, ambao sasa unapatikana bure, utafika wakati hautapatikana kabisa.


Ubarikiwe.

 
Top