KISA CHA MFALME NA MVUVI MWELEVU:*

Meria

Elder Lister
Staff member
*
Siku moja, Mfalme alipata hamu ya kula Samaki na akaamua kutembelea ufukweni mwenyewe. Siku hiyo ikawa Samaki hakuna Wavuvi wote wamekosa Samaki.

Wakati anarudi Nyumbani na wafuasi wake ndipo akakutana na Mvuvi mmoja tu aliyebahatika kupata *Samaki Watatu 3 tu*

Mfalme akataka kuwanunua Samaki wale, Mvuvi yule alikataa kuwauza Samaki wake.
Mfalme akaomba auziwe japo Samaki mmoja, lkn Mvuvi alikataa.

*"Mvuvi akamwambia Mfalme huyu Samaki Mmoja anaenda kumkopesha sijui kama Nitalipwa,*

*Na Samaki wa Pili, naenda kulipa Deni Na sijui kama nitalimaliza*

*Na huyu Samaki wa Tatu naenda kumtupa*

Mfalme akachukizwa Sana, kwa majibu yale ya MVUVI na akaamuru anyang'anywe wale samaki nae atupwe Gerezani.

Akiwa kwenye KASIRI lake, Mfalme akaamuru yule Mvuvi aletwe mbele yake ili amuhoji vizuri,
Kwanini amekataa kumuuzia wale samaki wakati ulisema mmoja unaenda kumkopesha tena hujui kama utalipwa!

Wa pili unaenda kulipa Deni na hujui kama utalimaliza!

Na Kisha Samaki wa Tatu unaenda kumtupa wakati mimi nina shida na Samaki!

Mvuvi akamjibu Mfalme kama ifuatavyo:
*Samaki wa kwanza:*
Huyu ninae kwenda kukopesha sijui kama nitalipwa naenda kuwapatia Wanangu,
Kwani kuwahudumia watoto hujui kama na wao watakuhudumia.
*Samaki wa Pili:*
Samaki huyu nilikuwa nakwenda kulipa Deni sijui kama nitalimaliza *Nawapelekea wazazi wangu.*
Kwa waliyonitendea siwezi kuwalipa hata niwape nini!

*Samaki wa Tatu:*
Samaki huyu niliyekuwa nakwenda kumtupa, *ilikuwa naenda kumpa Mke wangu*

Kwani wengi wao hawajui kushukuru wala kutosheka, hata uwape nini Siku akicharuka tu atasema hujamfanyia chochote tokea Umuoe.

Mfalme akamrudishia samaki.



.
 
Top