Jangili mamlakani - you can expect this if the wash wash brigade got to power...

Mwalimu-G

Chief Lister
Hukumu ya Sabaya yaibua hisia mseto Tanzania
15 Oktoba 2021
cv

CHANZO CHA PICHA,THECITIZEN
Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Kilimanjaro, Ole Sabaya, amehukumiwa kifungo cha miaka 30 kwenda jela, baada ya kukutwa na hatia ya makosa ya unyanganyi wa kutumia silaha.
Hukumu hiyo na kwa aina ya makosa aliyokutwa nayo ni ya kwanza katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni, hasa kwa kiongozi wa ngazi ya mkuu wa Wilaya nchini Tanzania. Mara baada ya hukumu hiyo kutolewa alasiri ya Oktoba 15, kumekua na mtazamo tofauti kwa wale waliokuwa wanamuunga mkono na wale waliotaka apewe adhabu kwa vitendo walivyokuwa wanaviita.
Paulo Mgosi, mkazi wa Arusha ameiambia BBC muda mfupi baada ya hukumu hiyo kwamba; 'mimi naona ni sawa , ni sahihi kwa matendo aliyofanya, ikiwa hivyo itakuwa fundisho kwa wengine watakaofanya matendo kama hayo wapigwe 30 kama Sabaya'.
Kauli hiyo ikaungwa mkono na mkazi mwingine wa Arusha, Richard Emanuel aliyesema; 'sikutegemea kiongozi kama yule, angeweza kufanya haya ambayo tunayasikia sasa, na kweli hukumu akaipata sikutegemea, kwakweli kuna viongozi wengine watajifunza'.
Kwenye mitandao ya kijamii pia kumekuwa na maoni mengi.
Tito Magoti, mmoja wa wanaharakati wa haki za binadamu nchini Tanzania, anasema hukumu hii ni kama imemshusha Sabaya, kutoka kuwa 'mwanamfalme mpaka mhuni'.
Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1
KADA yeye anasikitika kwa hukumu hiyo na kuandika kwamba analia na kumuonea huruma Sabaya akisema; ' Namlilia Sabaya, natumaini kila kitu kitakuwa sawa, namuonea huruma, natumaini rufaa labda zitamsaidia'
Albie akasema hilo ni fundisho la maisha, akitaka watu wawe na hofu ya Mungu.
Ruka Twitter ujumbe, 2

Mwisho wa Twitter ujumbe, 2
Sabaya alikuwa na nguvu gani kisiasa?
Ole Sabaya ni miongoni mwa wanasiasa vijana waliokuwa na nguvu wakati wa utawala wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano , marehemu John Magufuli. Baada ya kuwa kwenye nafasi ya mwenyekiti wa vijana wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi, (UVCCM) Arusha, kwa muda kuingia kwake kwenye nafasi ya Wilaya ilimtambulisha zaidi.
Nguvu zake kubwa zilionekana baada ya Rais Magufuli kumteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Julai 28, 201, akionekana kuendesha operesheni mbalimbali ambazo baadhi zilionekana kulalamikiwa na watu.
Mara kadhaa kwenye utendaji wake, alikuwa anaeleza anachokifanya ni maelekezo kutoka juu bila kutoa ushahidi, hata kama masuala hayo aliyokuwa akiyafanya yalionekana kwenda kinyume na sheria.
addd

CHANZO CHA PICHA,MWANANCHI
Sabaya aliteuliwa kuwa Mkuu wa wilaya katika wilaya lenye jimbo la Hai, lililokuwa chini ya Mkwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani, CHADEMA, na mwanasiasa mkubwa wa upinzani, Freeman Mbowe.
Wadadisi wa siasa wanasema uwepo wake Hai ulikuwa kama mkakati kuhakikisha nguvu za Mbowe, hazibaki zilivyo.
Aliwahi pia kutuhumiwa kwa makosa ya kujifanya afisa usalama, kesi ambayo alishinda na baadae akateuliwa kuwa mkuu wa Wilaya.
Makosa gani hasa yamemtia hatiani?
Sabaya na wenzake, Sylvester Nyegu na Daniel Mbura, walikuwa wakabiliwa na mashtaka matatu ya unyang'anyi wa kutumia silaha.
Shitaka la kwanza ilielezwa kwamba Februari 9, 2021 katika Mtaa wa Bondeni, Arusha, washtakiwa hao waliiba Sh2.769 milioni, mali ya mfanyabiashara Mohamed Saad.
Upande wa mashtaka ulidai kuwa kabla na baada ya kufanya wizi huo, washtakiwa waliwashambulia Numan Jasin, Harijin Saad Harijin, Bakari Msangi, Salim Hassan na Ally Shaban kwa kuwapiga kwa kutumia bunduki, ili kufanikisha wizi huo.
cv
 

The.Black.Templar

Chief Lister
Staff member
Yaani a crime that was committed in February this year, ata mwaka haujaisha and the guy has recieved justice so swiftly......hapa Kenya joh....how long has it taken obados case to just start....they impeached Waititu because of overwhelming evidence but the case is yet to even start....shait!
 
Top