Biblia inaposema hakitaingia kinyonge ina maana gani?

john7

Lister
SWALI; Naomba kuuliza katika ufunuo 21:27 kwamba hakitaingia kilicho kinyonge hili neno kinyonge linamaanisha nini? Je ni watu dhaifu mfano vilema?

Ufunuo wa Yohana 21:27
[27]Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.

images (69).jpeg


JIBU : “Kinyonge” kinachozungumziwa hapo si mtu mlemavu, kama ingekuwa hivyo Bwana Yesu asingesema..kiungo chako kimoja kikikukosea king’oe ni heri uingie mbinguni mlemavu kuliko kuwa viungo vyako vyote na kuishia kuzimu.(Mathayo 5:29-30)

Umeona sio mlemavu anayezungumziwa hapo

Kitu kinyonge sikuzote ni kitu kisichokuwa na nguvu ya kustahimili mtikisiko fulani aidha mapigano,ugonjwa,dhoruba n.k.

Vivyo hivyo katika roho mtu asiyekuwa na nguvu ya kuishinda dhambi huyo ni sawa na mnyonge. Na ndio maana Bwana Yesu alisema maneno haya..

Mathayo 11:12
[12]Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.

Huu si wakati wa kuikumbatia dhambi..na kusema kwamba mimi siwezi kuushinda ulevi..au mimi siwezi kuushinda uzinzi..au mimi siwezi kuushinda wizi, mimi siwezi kushinda vimini…ni wajibu wako kushindana mpaka ushinde..hicho sio kisingizio cha Mungu kukusamehe siku ile.

Na ili tuweze kufikia hapo ni lazima tumaanishe kabisa kutubu na kumfuata Kristo kwa mioyo yetu yote.Ndipo atokee kutusaidia kuyashinda hayo yaliyosalia.

Lakini ukiwa ni mtu wa kukiri tu mdomoni lakini moyoni upo mbali na Mungu..kamwe huwezi kuishinda dhambi hata kidogo.

Na huo ndio unyonge unaozungumziwa ambao utakufanya ushindwe kuiona mbingu siku ile.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa mafundisho whatsapp :+255 693036618
 

Attachments

Top